Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi DR Congo: Fayulu ataja uchaguzi kuwa wenye 'vurugu'

Uchaguzi DR Congo: Fayulu Ataja Uchaguzi Kuwa Wenye 'vurugu' Uchaguzi DR Congo: Fayulu ataja uchaguzi kuwa wenye 'vurugu'

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Martin Fayulu, mmoja wa wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amepiga kura yake katika mji mkuu, Kinshasa.

Anasema upigaji kura unaendelea vizuri Kinshasa lakini "hali ni ya vurugu" katika maeneo makubwa ya vijijini nchini DR Congo.

"Nina watu wangu wanaozunguka nchi nzima na hakuna kilicho tayari," Bw Fayulu anasema muda mfupi baada ya kupiga kura katika mkoa wa Gombe.

Kiongozi wa chama cha ECiDé anatishia kukataa matokeo ya uchaguzi ikiwa raia hawataweza kupiga kura.

Bw Fayulu, ambaye alikuwa mshindi wa pili katika uchaguzi uliopita, anasema bado ana imani kwamba atashinda kinyang'anyiro cha urais.

Chanzo: Bbc