Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi Afrika Kusini: Jinsi upigaji kura unavyofanyika

Uchaguzi Afrika Kusini: Jinsi Upigaji Kura Unavyofanyika Uchaguzi Afrika Kusini: Jinsi upigaji kura unavyofanyika

Wed, 29 May 2024 Chanzo: Bbc

Kwa mara ya kwanza, wapiga kura watapatiwa karatasi tatu za kupigia kura watakapoingia kwenye chumba cha kupigia kura.

Kura ya kwanza itakuwa na orodha ya vyama vinavyowania viti 200 vya ubunge nchi nzima.

Kura ya pili itaorodhesha vyama na wagombea huru, katika majimbo yanayowania viti vingine 200 vya ubunge. Hii ni mara ya kwanza kwa kura hii kuanzishwa ili kuwapa nafasi wagombea huru kugombea ubunge, na kuimarisha uwakilishi wa majimbo katika chombo cha kutunga sheria.

Hakuna uchaguzi wa moja kwa moja wa rais. Bunge jipya litachagua rais, ambaye kwa kawaida ndiye kiongozi wa chama kilicho na wabunge wengi.

Kura ya tatu ni ya mabunge ya majimbo, moja kwa kila majimbo tisa ya Afrika Kusini. Wapiga kura katika kila jimbo wanapigia kura bunge lao, na wakati huu wataweza kupiga kura kwa wagombea huru, badala ya vyama pekee.

Mikoa ina bajeti kubwa, na inawajibika kwa mambo kama vile elimu na afya, pamoja na serikali ya kitaifa.

Chanzo: Bbc