Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchaguzi Afrika Kusini: Chama cha EFF cha Julius Malema chapata pigo kubwa

Uchaguzi Afrika Kusini: Chama Cha EFF Cha Julius Malema Chapata Uchaguzi Afrika Kusini: Chama cha EFF cha Julius Malema chapata pigo kubwa

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Baada ya chama tawala cha African National Congress (ANC), aliyeshindwa zaidi katika uchaguzi huu ni chama chenye msimamo mkali cha Economic Freedom Fighters (EFF), kinachoongozwa na Julius Malema.

EFF imepoteza hadhi yake kama chama cha pili kwa ukubwa nchini Afrika Kusini kwa mshiriki wa mara ya kwanza - chama kipya cha Rais wa zamani Jacob Zuma, Umkhonto weSizwe (MK).

Huku takriban matokeo yote yakitangazwa, EFF imesimama kwa asilimia 9, chini kutoka 11 iliyopata katika uchaguzi uliopita.

Kura za MK zimesimama kwa asilimia 15, huku chama hicho kikipata kura kutoka kwa ANC na EFF.

Hili ni pigo kubwa kwa Malema na EFF.

Ana matarajio ya siku moja kuwa rais wa Afrika Kusini, na alikuwa na matumaini kwamba EFF itachukua nafasi ya pili katika uchaguzi huu, na kumfanya kuwa kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha upinzani.

Hata hivyo, ndoto hiyo ilikatizwa na wapiga kura.

Chanzo: Bbc