Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchafuzi wa hewa waua milioni 1.1 Afrika

Pollution Uchafuzi wa hewa waua milioni 1.1 Afrika

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa utafiti wa mazingira uliofanyika mwaka 2019, umeonesha kuwa uchafuzi wa hewa umesababisha jumla ya vifo milioni 1.1 barani Afrika.

Inaelezwa kuwa vifo 697,000 vimesababishwa na uchafuzi wa hewa unaotokana na shughuli za majumbani hasa kutoka kwenye majiko ya kupikia.

Hata hivyo inaelezwa kuwa uchafuzi huo wa majumbani unapungua kwa kasi kubwa huku ule wa nje ukiongezeka jambo ambalo linakadiriwa kuja kuwa tatizo kubwa siku zijazo, hii ni kwa mujibu wa Profesa Pushpam Kumar aliyeongoza utafti huu ulio chini ya Mpango wa mazingira wa Umoja wa Mataifa.

Uchafuzi wa hewa umebainika kuwa chanzo kikuu cha pili cha vifo Afrika, unatajwa kuwa tishio kubwa la usalama wa afya, maendeleo ya jamii. huku jumla ya asilimia 16.3 ya vifo vikisababishwa na uchafuzi huo.

Uchafuzi wa hewa wa nje unachochewa sana shughuli za kiuchumi kama vile viwanda na jumla ya vifo 394,000 vimetokana na hewa chafu inayotengenezwa viwandani.

Watafti hawa wameeleza kuwa uchafuzi wa hewa unasababisha vifo vingi kuliko ajali za barabarani, matumizi ya pombe na tumbaku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live