Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubora wa bidhaa Burundi waongeza mauzo nje

698c33426b4b7fa61aae3efa75a743a9 Ubora wa bidhaa Burundi waongeza mauzo nje

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BIDHAA zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi zimepata soko kubwa baada ya kuboreshwa viwango vya ubora.

Mafanikio hayo yamepatikana baada ya serikali kupata vifaa vya maabara vya kudhibiti ubora wa bidhaa kwa ajili ya wakala anayehusika na usanifishaji na udhibiti wa ubora (BBN) nchini.

Vifaa hivyo vilivyotolewa chini ya Mfumo wa Usaidizi wa Ujumuishaji wa Jumuiya ya Comesa (RISM), ni vya kisasa vya kuhakikisha ubora wa viwango vya bidhaa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Biashara, vifaa hivyo vimesaidia wazalishaji kupata vyeti vya ubora na kupunguza gharama tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Wizara hiyo imesema idadi kubwa ya wazalishaji wa maziwa sasa wanaweza kupeleka bidhaa zao kwa uthibitisho na kwamba hapo awali ni idadi ndogo tu ya bidhaa za bidhaa zilisafirishwa nje ya nchi kutokana na kukosekana uthibitisho wa ubora.

Chini ya mpango wa RISM ambao fedha zake zinatokana na Jumuiya ya Ulaya (EU) kupitia Mfuko wa Marekebisho wa Comesa(CAF), Burundi imepokea msaada wa kifedha wa karibu dola za Marekani milioni 16 kwa kipindi cha 2010-2020.

Kupitia msaada kutoka kwa RISM, Sera ya Ubora ya Kitaifa ilitengenezwa mwaka jana na kwa sasa inasubiri kupitishwa na Baraza la Mawaziri.

Chanzo: habarileo.co.tz