Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uamuzi wa ICJ:Mahakama imesita kuomba usitishaji mapigano mara moja

Uamuzi Wa ICJ:Mahakama Imesita Kuomba Usitishaji Mapigano Mara Moja Uamuzi wa ICJ:Mahakama imesita kuomba usitishaji mapigano mara moja

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama haikukubaliana na ombi la Afrika Kusini la kusitisha mapigano mara moja huko Gaza - jambo ambalo litawakatisha tamaa Waafrika Kusini na Wapalestina vile vile.

Lakini kwa kiasi kikubwa majaji 17 wa mahakama hiyo waliamua, pamoja na hatua nyingine, kwamba Israel inapaswa kufanya kila iwezalo ili kuepuka kuwaua Wapalestina, kuwasababishia madhara makubwa ya mwili au kiakili au kuweka hatua zinazokusudiwa kuwazuia wanawake wa Kipalestina kujifungua.

Huu sio uamuzi wa mwisho wa mahakama kuhusu mauaji ya halaiki – ambayo huenda ikachukua miaka kadhaa.Lakini hatua zinazotakiwa kufanyika leo zimeundwa ili kuhakikisha kwamba wakati majaji wanazingatia shtaka la msingi la Afrika Kusini dhidi ya Israel, Wapalestina wa Gaza wanafurahia kiasi fulani cha ulinzi.

Israeli lazima sasa iamue jinsi ya kujibu.Maamuzi ya ICJ ni ya lazima, lakini hakuna utaratibu wa utekelezaji.Israeli wangeweza kuchagua kuwapuuza waamuzi kabisa.Lakini huku juhudi za kidiplomasia sasa zikionekana kulenga uwezekano wa usitishaji mapigano kwa muda wa miezi miwili, na juhudi bado zinafanywa kuboresha utiririshaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza, Israel inaweza kusema kuwa tayari inachukua hatua kukidhi matakwa ya mahakama.

Majaji waliamua kupendelea ubinadamu, asema waziri wa Palestina

Baadhi ya majibu ya haraka sasa kutoka kwa waziri wa mambo ya nje wa Palestina, ambaye amekaribisha hatua za muda zilizoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

"Majaji wa ICJ walitathmini ukweli na sheria, waliamua kupendelea ubinadamu na sheria za kimataifa," Riyad Al-Maliki anasema, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Al-Maliki anatoka Mamlaka ya Palestina ambayo inaendesha sehemu za Gaza na Ukingo wa Magharibi, na ni mpinzani wa Hamas.

Chanzo: Bbc