Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uagizaji bidhaa Kenya na Uganda washuka kwa 34%

Uganda Pic Uagizaji bidhaa Kenya na Uganda washuka kwa 34%

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka nchini Uganda imetajwa kushuka kwa zaidi ya asilimia 4 kwa takribani miezi nane kufuatia vita ya kibiashara iliyopo baina ya Kenya na Uganda ambayo kwa kiasi kikubwa imeathiri mfumo mzima wa usafirishaji bidhaa.

Nayo taarifa kutoka Benki kuu ya Kenya inaonesha kuwa kiasi cha uagizaji bidhaa kutoka nchini Uganda kimeshuka kutoka dola milioni 29 sawa na bilioni 66.70 za kitanzania mwezi Februari hadi dola milioni 19 sawa bilioni 43.7 za kitanzani kufika mwezi Oktoba.

Mataifa hayo mawili yapo kwenye mgogoro wa kibiashara kwa miaka miwili mara baada ya Kenya kupiga marufuku pamoja na kuongeza kodi kwenye bidhaa ya maziwa yanayotoka nchini Uganda.

Hata hivyo ujumbe wa Kenya upo tayari kufanya mazungumzo na Uganda ili kufikia hatma ya mzozo huo amabao unaathiri uchumi wa mataifa yote mawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live