Utafiti mpya uliofanywa na taasisi ya Afrika Kusini ya Ichikowitz Family umeonesha kuwa zaidi ya asilimia 52 ya vijana 4,500 [waliohusika kwenye utafiti huo] wenye umri wa kati ya miaka 18-24 wanatamani kuondoka Afrika na kutorejea tena.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa mwaka 2022 na kuchapishwa kwa kichwa cha habari “African Youth Survey 2022” unaonesha kuwa vijana hao wanafikiria kuondoka Afrika kwenye miaka michache ijayo huku hali ngumu ya kiuchumi [Afrika] na fursa za elimu sambamba na ajira zikiwa sababu kubwa zinazowashawishi vijana hao.
Shirika la utangazaji la Uingereza, BBC limesema limezungumza na vijana watano kutoka Nigeria na Afrika Kusini ambao wamekiri kutamani kuondoka Afrika huku wakiongezea sababu za kiusalama ikiwemo utekwaji nyara wa binadamu kwenye nchi hizo kuchangia shauku ...