Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

USAID na WFP zasitisha misaada ya chakula Tigray

USAID Na WFP Zasitisha Misaada Ya Chakula Tigray USAID na WFP zasitisha misaada ya chakula Tigray

Thu, 4 May 2023 Chanzo: Voa

Shirika la misaada na maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID), na mpango wa chakula duniani (WFP) Jumatano yametangaza kwamba yanasimamisha msaada wa chakula kwa mkoa ulio athirika na vita wa Tigray baada shehena ya msaada kupelekwa katika masoko ya kawaida.

Samanta Power ambaye ni mkuu wa USAID, ambalo ni shirika kuu la misaada ya kimataifa la serekali ya Marekani, amesema kwamba wameamua kufanya uamuzi mgumu wa kusimamisha msaada wa chakula wa USAID mkoani Tigray mpaka watakapo toa taarifa zaidi.

Shirika hilo hivi karibuni lilianzisha msaada mwingine wa chakula uliokuwa na dhamirra ya kupelekwa kwa watu wa Tigray ambao wanakabiliwa na hali ya ukame lakini ulihamishwa na kuuzwa kwenye masoko ya kawaida amesema Samantha Power katika taarifa yake.

WFP pia imesema imesimamisha usambazaji wa chakula mkoani Tigray baada kutambua tatizo la vyakula kupelekwa kwenye kusiko stahili.

Chanzo: Voa