Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNICEF: watoto mil.3.6 wanahitaji msaada Afrika Mashariki na Kusini mwa bara

UNICEF Watoto mil.1.5 wanatatizo la uzito mdogo Afrika Mashariki na Kusini

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF, Limesema, takribani watoto milioni 3.6 wanahitaji msaada wa dharuda na kuongeza kua idadi hiyo hawafikiwi kwa wakati ili kuokoa maisha yao au kuwaepusha na uharibifu wa kudumu.

Akizungumzia utafiti wa shirika hilo uliofanywa kwenye mataifa ya Angola, Ethiopia, Sudan Kusini, Madagascar, Somalia, Kenya, na Msumbiji, Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Mohamed M. Fall amesema watoto katika kanda ya Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika wamekua wahanga wa matukio mbalimbali hali inayopelekea kukosa msaada kwa haraka.

"Hakuna kitu kinachoumiza zaidi kuliko kuona watoto wakiteseka kutokana na unyafuzi mkali wakati tunajua kuwa ungeweza kuzuiwa na kutibiwa. Shukrani kwa msaada wa wafadhili na washirika wetu, tumefikia baadhi ya matokeo bora na hadithi za mafanikio; lakini athari za COVID19, mabadiliko ya tabianchi na migogoro vinaleta sintofahamu ya upatikanaji wa haraka wa rasilimali, na wakati wa kuchukua hatua ni sasa."

UNICEF inasema kwa sasa, familia katika eneo lote zinakabiliana na migogoro mingi, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa viwango vya uhaba wa chakula, kuzorota kwa uchumi, milipuko ya magonjwa, mizunguko isiyo ya kawaida ya mafuriko na ukame, na migogoro. Mamilioni ya watu wanalazimika kupunguza wingi au ubora wa chakula wanachokula ili waendelee kuishi. Mara nyingi, familia hulazimika kufanya yote mawili.

Shirika hilo la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa linaeleza kuwa hali katika eneo hilo tajwa bado ni mbaya na usumbufu wowote wa operesheni ya kibinadamu ambazo tayari zimeelemewa, inaweza kuzidisha kile ambacho tayari ni janga la lishe ya muda mrefu.

UNICEF inatafuta dola za Marekani milioni 255 ili kuongeza hatua zake za dharura kutatua tatizo la lishe katika nchi zilizopewa kipaumbele katika Mashariki na Kusini mwa Afrika mwaka 2022, na kusaidia watoto kwa huduma za lishe za kutosha na za kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na matibabu ya unyafuzi mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live