Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNICEF: Mamilioni ya watoto wanashindwa kwenda shule Sudan

Unicef Uniceffffff UNICEF: Mamilioni ya watoto wanashindwa kwenda shule Sudan

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vita na machafuko yanayoendelea nchini Sudan yamesababishha mamilio ya watoto wa nchi hiyo kushindwa kwenda shule.

Mzozo ulioanza katikati ya mwezi Aprili mwaka huu kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka umeufanya mfumo wa elimu wa nchi hiyo kufikia ukingo wa kuporomoka.

Zaidi ya shule 10,000 zimefungwa, huku zaidi ya shule 170 zinatumika kama makaazi ya dharura kwa wale waliokimbia makazi yao kutokana na mapigano.

Jaafar Abbakar, mzazi wa watoto wanne, ni mmoja wa wale wanaoishi katika makazi ya shule. Yeye na familia yake walikimbilia jimbo la Gederaf kutoka Umbada, magharibi mwa Omdurman. Anasema hata kama shule zitafunguliwa mwaka huu, watoto wake hawako tayari kurejea.

"Ni vigumu kwa sababu za kisaikolojia. Katika hali kama hizi, mtu hawezi kwenda shule. Hakuna dalili za kuahidi kwamba vita vitaisha,” anasema.

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) unasema kuwa, hata kabla ya vita kuzuka karibu watoto milioni saba walikuwa tayari hawaendi shule nchini Sudan kutokana na umaskini na ukosefu wa utulivu. Sasa watoto zaidi ya milioni sita na nusu hawaendi shule kutokana na mapigano huku zaidi ya watoto milioni tano wameathiriwa na kufungwa kwa shule.

Umeshaingia mwezi wa sita tangu vita baina ya majenerali wa kijeshi vianze huko Sudan. Vita hivyo vya vya kikatili vinaendelea kusababisha mateso yasiyokadirika, vinahatarisha maisha, kuwafukuza mamilioni ya makazi yao, na kusababisha vifo hata katika maeneo yaliyoko mbali na mstari wa mbele wa mapigano.

Zaidi ya watu 9,000 wameshauwa, milioni 5.6 wamekimbia makazi yao na magonjwa kama ya kipindupindu yameeneo, viwanda vinaharibiwa na miundombinu yote imesambaratishwa kutokana na vita baina ya majenerali Abdel Fattah al-Burhan na Mohamed Hamdan Daglo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live