Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNHCR: Zaidi ya watu milioni moja wakimbia makazi Sudan

Idadi Ya Wakimbizi Wa Ndani Nchini Sudan Yafikia 700,000 UNHCR: Zaidi ya watu milioni moja wakimbia makazi Sudan

Sat, 20 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) amesema kuwa zaidi ya watu milioni moja wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano nchini Sudan hadi sasa.

Matthew Saltmarsh ameuambia mkutano wa Geneva kwamba idadi hiyo ni pamoja na takriban watu 843,000 ambao ni wakimbizi wa ndani ya nchi na karibu watu 250,000 ambao wamekimbia na kuvuka mipaka ya Sudan

Takriban watu 1,000 wameuawa na karibu milioni moja wamekimbia makazi yao nchini Sudan tangu vita kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan ambaye pia ni kiongozi wa Sudan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, anayeongoza Kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF) kuzuka kati kati ya mwezi Aprili.

Wakimbizi wamemiminika katika nchi jirani kama Chad, Ethiopia, na Sudan Kusini, ambazo zote zinakabiliwa na majanga makubwa ya binadamu.

Tangu kuanza kwa mzozo huo, Misri imepokea idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan kuliko nchi nyingine yoyote ambapo Wasudani waliokimbilia nchini humo ni karibu 110,000.

Wakati huo huo Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu, Martin Griffiths, amelaani kile alichokitaja kuwa ukiukwaji wa mara kwa mara na mkubwa wa makubaliano yaliyofikiwa wiki moja baina ya pande zihasimu katika mzozo wa Sudan ya kulinda maisha ya raia, harakati za misaada ya kibinadamu na miundombinu.

Siku chache zilizopita Umoja wa Mataifa na wadau wake walifanyia marekebisho ombi la msaada kwa nchi hiyo na sasa linafikia dola bilioni 3 kwa ajili ya kusaidia mamilioni ya watu nchini humo na mamia ya maelfu ya wengine waliokimbilia nchi jirani.

Uzinduzi wa ombi hilo lililorekebishwa ulifanywa kwa pamoja Jumatano huko Geneva, Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live