Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNHCR: Mtoto mmoja kati ya wawili wakimbizi ana utapiamlo Ethiopia

Ethiopiaaa Watoto Wakimbizi UNHCR: Mtoto mmoja kati ya wawili wakimbizi ana utapiamlo Ethiopia

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limefichua kuwa, mtoto mmoja kati ya kila watoto wawili wakimbiza ana utapiamlo nchini Ethiopia.

Katika ripoti yake ya karibuni kabisa iliyosambazwa jana Alkhamisi, UNHCR imesema kuwa, kuna nakisi kubwa katika utoaji wa huduma za lishe kwa wakimbizi nchini Ethiopia na kwamba utafiti wa shirika hilo uliofanywa kwenye kambi na maeneo 21 kote Ethiopia unaonesha kuwa, mtoto mmoja kati ya kila watoto wawili wakimbizi, wenye umri wa hadi miaka 6 anasumbuliwa na utapiamlo.

Takwimu kutoka UNHCR zinaonesha kuwa takriban watoto 95,334 kati ya 203,371 (laki mbili na 3371), ikiwa ni asilimia 46.9 ya watoto hao wakimbizi wamegundulika kuwa na matatizo ya utapiamlo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, miongoni mwa matatizo ya watoto hao ni pamoja na kudumaa, uzito mdogo na upungufu wa virutubishi.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi limeongeza kuwa, akina mama wana upungufu mwingi, wanashindwa hutoa lishe bora kwa watoto wachanga wa chini ya miezi 6 na wanashindwa pia kunyonyesha mapema.

Mbali na wakimbizi wa ndani, kuna wakimbizi wengine wanaotoka nje ya Ethiopia. Mwaka jana shirika hilo lilitangaza kwenye ripoti yake kwamba karibu watu laki moja waliokimbia mapigano huko Somaliland; eneo lililojitenga la kaskazini mwa Somalia, wamekimbilia Ethiopia na hali yao ni mbaya sana.

Taarifa ya shirika hilo la Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa ilisema kwenye ripoti yake kwamba inakadiria kuwa watu 98,000 waliwasili katika wilaya tatu za Ethiopia zinazopakana na eneo la Somaliland kwenye kipindi cha mwezi mmoja na walikuwa wanahitajia misaada ya haraka ya kibinadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live