Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNHCR: Mgogoro wa Niger kusababisha maafa yala kibinadamu

Unhcr Niger UNHCR: Mgogoro wa Niger kusababisha maafa yala kibinadamu

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi UNHCR limeonya kuwa, mzozo wa Niger huenda ukapelekea kuibuka janga la kibinadamu katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Hayo yanatangazwa wakati kukiwa na mashambulizi kutoka makundi yenye silaha yasiyo ya serikali pamoja na vikwazo vilivyowekwa na ECOWAS kwenye taifa hilo lisilo na bandari.

Inadhari hiyo ya UNHCR inatolewa wakati kukiwa hakuna suluhisho la kisiasa linaloonekana baada ya jeshi kkutwaa madaraka kufuatia mapinduzi ya mwezi uliopita wa Julai.

Tangu kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Bazoum, aliyechaguliwa kidemokrasia hapo Julai 26, kumekuwa na hali ya taharuki, amesema mwakilishi wa UNHCR nchini Niger Emmanuel Gignac.

Ameongeza kusema kwamba ni vigumu kubashiri hali itakavyokuwa, na kwamba UNHCR na UN wameweka mikakati ya kukabiliana na dharura inayoweza kutokea.

Amesema kwamba ghasia na mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha na hasa karibu na mpaka wa Mali na Burkina Faso yamesababisha zaidi ya watu 20,000 kuondoka makwao ndani ya mwezi mmoja uliopita.

Jeshi limechukua madaraka nchini Niger huku kukiwa na wimbi kubwa la chuki dhidi ya Wafaransa, ambapo watu wa Niger wanaishutumu nchi hiyo ya Ulaya kwa kuingilia masuala yao ya ndani.

Tangu kuchukua mamlaka, Waniger mara kadhaa wamejitokeza kwa nguvu kuonyesha uungaji mkono wao kwa viongozi wa kijeshi na kupinga tawala za zamani ambazo wamezitaja kuwa vibaraka wa Magharibi.

Mapema mwezi huu, maelfu ya waandamanaji dhidi ya Magharibi waliingia barabarani kupinga mipango ya mataifa ya Afrika Magharibi kupeleka kikosi cha kijeshi nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live