Shirika la Umoja wa Mataifa la kitamaduni UNESCO limeongeza chakula cha kitamaduni kutoka nchini Senegal kwenye orodha ya urithi wa utamaduni duniani kufuatia upekee wa chakula hicho.
Wizara ya utamaduni ya Senegal iliomba kujumuisha chakula hich katika orodha hiyo kwakuwa hutumiwa sana nchi hiyo ya ukanda wa Afrika Magharibi
"Thiebou dieune" inamaanisha "wali na samaki" katika lugha kuu ya Kiwolof nchini Senegali. Mara nyingi hutayarishwa kwa mboga mboga kama vile muhogo au nyanya, na kuliwa wakati wa chakula cha mchana.
Chakula hicho kinaaminika kuanza kutumika Kaskazini mwa Jiji la Saint Louis nchini humo.