Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNECA yasikitishwa na ongezeko la ajali za barabarani Afrika

Sakamu Ajali.jpeg UNECA yasikitishwa na ongezeko la ajali mbaya za barabarani barani Afrika

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mtendaji wa Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) Claver Gatete ameelezea wasiwasi wake mkubwa kutokana na ongezeko la ajali mbaya za barabarani barani Afrika.

Akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Ushirikiano wa Usalama Barabarani, Gatete amesema kuwa, kiwango kikubwa cha vifo vya barabarani barani Afrika ni cha kutisha, hasa kwa vile bara hilo lina takriban asilimia 3 tu ya magari yote duniani.

Amesema, Afrika inahitaji kuungwa mkono katika kuendeleza usimamizi wake wa usalama barabarani ili kupunguza kasi ya ajali mbaya za barabarani ambazo zinaathiri maendeleo ya bara hilo.

Aidha amesema: "Inatisha pamoja unapoona kwamba vifo vinavyotokana na ajali za barabarani barani Afrika viliongezeka kwa asilimia 15 kati ya 2019 na 2020."

Maafa ya moja ajali mbaya za barabarani nchini Nigeria

Kwa upande wake, Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kiwango cha vifo vya barabarani katika bara hilo kuwa kuwa 26.6 kwa kila watu 100,000 ikilinganishwa na 17 Kusini Mashariki mwa Asia, 9.3 barani Ulaya na wastani wa 17.5 kote ulimwenguni, wakati kama ilivyotangazwa, bara la Afrika lina asilimia 3 tu ya magari yote duniani.

Ripoti ya Hali ya Usalama Barabarani ya WHO ya mwaka 2023 iliyozinduliwa siku chache zilizopita inaonesha kuwa, takriban watu milioni 1.19 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, huku watu wanaojeruhiwa kutokana na ajali hizo za barabarani wakiwa ndicho chanzo kikuu cha vifo vya watoto na vijana wenye umri wa kati ya miaka 5-29. barani Afrika.

Vilevile Gatete ameutaka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usalama Barabarani (UNRSF) kufikiria kuwekeza zaidi katika miradi barani Afrika kutokana na ukubwa wa matatizo ya usalama barabarani barani humo.

Aidha ametoa mwito kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa kusaidia kuboresha utamaduni wa kutegemea takwimu za usafiri wa nchi kavu barani Afrika ili kuzisaidia taasisi zinazojishughulisha na usalama wa barabarani barani humo kuweka mikakati mizuri ya kazi zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live