Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yatoa tathimini idadi ya vifo vita ya Sudan

Marekani Inaitaka RSF Ya Sudan Kuacha Kushambulia Maeneo Ya Raia UN yatoa tathimini idadi ya vifo vita ya Sudan

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 12,000 wameuawa nchini Sudan katika vita vya wenywe kwa wenyewe vilivyoanza Aprili 15 mwaka huu huku hali ikiendelea kuwa mbaya.

Hayo ni kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ambayo katika ripoti yake ya Alhamisi imesema vifo hivyo ni pamoja na "watu 1,300 waliouawa kati ya Oktoba 28 na 24 Novemba.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu imeongeza kuwa, mzozo huo umesababisha takriban Wasudan milioni 6.6 kukimbia makazi yao, huku watoto wakiwakilisha takriban nusu ya watu waliokimbia makazi yao nchini humo.

OCHA imesema: "Sudan sasa ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu waliokimbia makazi yao na pia ni nchi yenye janga kubwa zaidi la kuhama watoto duniani."

Sudan imekumbwa na vita kati ya Jeshi la Kitaifa likiongozwa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa Baraza la Utawala la nchi hiyo, na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vikiongozwa na jenerali muasi Mohammad Hamdan Dagalo (Hemedti).

Hitilafu kati ya al-Burhan na Dagalo zilijitokeza baada ya kusainiwa mkataba wa kuunda kipindi cha mpito na kukabidhiwa madaraka kwa raia. Dagalo anataka wapiganaji wa RSF waingizwe jeshini lakini al Burhan anapinga pendekezo hilo. Mikataba kadhaa ya kusitisha mapigano iliyosimamiwa na Saudia imeshindwa kukomesha ghasia hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live