Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yatoa hati kukamatwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Afrika Ya Kati Rais UN yatoa hati kukamatwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Maalumu ya Jinai (CPS) inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imesema, imetoa hati ya kukamatwa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu unaodaiwa kufanywa na jeshi wakati wa uongozi wake. Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo yenye makao yake mjini Bangui imebainisha kuwa, uhalifu unaodaiwa kufanywa ni pamoja na mauaji, kutoweka kwa kulazimshwa, utesaji, ubakaji na vitendo vingine visivyo vya kibinadamu, vilivyofanywa kati ya mwaka 2009 na 2013.

Uhalifu huo inasemekana ulifanywa na walinzi wa rais wa Bozize na vikosi vingine katika gereza la kiraia na katika kituo cha mafunzo ya kijeshi katika mji wa Bossembele.

Majaji wa CPS wamesema, kutokana na ushahidi mkubwa na madhubuti uliopo dhidi ya Bozize kuna uwezekano wa kumbebesha dhima ya kutenda jinai katika nafasi yake kama kiongozi wa ngazi ya juu na kiongozi wa kijeshi. Jaji wa CPS

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, waranti huo wa kimataifa dhidi ya Bozize ulitolewa tangu Februari 27, lakini uliwekwa hadharani jana Jumanne.

Bozize mwenye umri wa 77, alitawala Jamhuri ya Afrika ya Kati kuanzia Machi 2003 hadi Machi 2013 alipopinduliwa. Alinyakua madaraka pia kupitia mapinduzi ya kijeshi, na anaishi uhamishoni nchini Guinea-Bissau tangu Machi 2023.

Mahakama ya CPS imeitaka Guinea-Bissau kutoa ushirikiano wa kumkamata na kumkabidhi mtuhumiwa huyo.

Septemba mwaka jana, Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilimhukumu Bozize hukumu ya kifungo cha maisha jela na kazi ngumu kwa makosa ya kudhoofisha usalama wa ndani wa taifa na kuhusika na mauaji kadhaa.

Bozize sasa anahudumu kama mratibu wa Muungano wa Wazalendo wa Mabadiliko (CPC), muungano mkuu wa waasi ulioundwa mwaka 2020 kwa lengo la kumpindua mfuatizi wake, Faustin Archange Touadera.

Mahakama ya CPS iliyoanzishwa mwaka 2015 kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa inasimamia uchunguzi wa uhalifu wa kivita uliofanywa tangu mwaka 2003 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo ilijipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni Ufaransa mwaka 1960.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live