Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yathibitisha kuachiwa watoto waliotekwa na Al-shabab Msumbiji

Child Army Serikali yawaokoa watoto waliotekwa na Al-Shabab Msumbiji

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Msumbiji imewaokoa watoto waliokouwa wametekwa nyara kisha kupewa kwa lazima mafunzo ya kijeshi na kundi la kijihadi la Al-Shabab kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa hii imetolewa nja Umoja wa Mataifa, kupitia kitendo cha watoto UNICEF, ambao hawakuweka wazi jumla ya idadi ya watoto waliowanusuru kwa kuhofia kuharibu mpango waliouweka wa kukamilisha zoezi hilo.

"Tayari watoto wameshaokolewa lakini si kuachiwa, wamenusuriwa na vikosi vya serikali ya Msumbiji" amesema James Elder Msemaji wa UNICEF.

Kundi hilo la kijihadi linalofungamana na Dola ya Kiislamu IS, limevamia mkoa wa Cabo Delgado wenye utajiri mwingi wa gesi nchini humo tangu mwaka 2017 na kwa kipindi hicho chote limekuwa likifanya vitendo vya ugaidi na uhalifu mkubwa katika vijiji na miji nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live