Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yatangaza hali ya hatari Nigeria

UN NIGERIA UN yatangaza hali ya hatari Nigeria

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria ambaye pia ni mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini humo Matthias Schmale amesema zaidi ya watu milioni 4.1 kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wanahitaji msaada wa haraka wa chakula katika msimu wa mwambo utakao anza hivi karibuni.

Akihutubia kikao cha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi Schmale amesema watu hao ambao wameteseka kutokana na vita kwa miaka 12 wana uhitaji mkubwa na wa haraka wa misaada ya kibinadamu hususan katika ukanda wa majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe ambapo takwimu za mwaka huu wa 2022 zinaonesha kuwa watu wenye uhitaji ni milioni 8.4.

“Uhaba wa chakula umeonekana dhahiri katika majimbo haya hususan wakati huu shughuli za uendeshaji zikiwa zina uhitaji mkubwa wa ufadhili”, amesema Schmale na kutolea mfano “katika jimbo la Yobe, familia hazijapokea msaada wa chakula kwa takriban miezi minane, baadhi ya watu wanakosa chakula kwa siku kadhaa".

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria ameziomba nchi wanachama na jumuiya za kimataifa kusaidia kwa haraka ili kuokoa maisha ya wahitaji.

Mwezi Machi mwaka huu wa 2022 chombo cha kutambua maeneo yaliyo hatarini kutokana na uhaba wa chakula “Cadre Harmonisé” katika ukanda wa Sahel na Afrika Magharibi kilibainisha kuwa kati ya mwezi Juni hadi Septemba watu milioni 4.1 watakuwa na uhaba wa chakula.

Imeelezwa pia kwamba, takriban watoto milioni 1.74 walio chini ya umri wa miaka mitano wanatarajiwa kukumbwa na utapiamlo uliokithiri huko kaskazini-mashariki ya Nigeria na kati ya hao, zaidi ya 300,000 wanatarajiwa kukabiliwa na utapiamlo mkali na wako katika hatari kubwa ya kufariki ikiwa hawatapokea matibabu ya haraka

Chanzo: www.tanzaniaweb.live