Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yataka ushirikiano zaidi kwa ajili ya kurejesha utulivu nchini Somalia

Watu 6 Wauwawa, 10 Wajeruhiwa Katika Shambulizi Somalia UN yataka ushirikiano zaidi kwa ajili ya kurejesha utulivu nchini Somalia

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya serikali ya Somalia na Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika (ATMIS) kwa kurejesha utulivu nchini Somalia na wakati huo huo umehimiza kufanyika juhudi zaidi za kurejesha usalama katika kona zote za nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa barani Afrika, Martha Pobee, ambaye Jumamozi alimaliza ziara yake ya siku tatu nchini Somalia amesema kwenye matamshi yake ya karibuni kabisa kwamba, wakati wa ziara yake hiyo aliwahakikishia viongozi wa ATMIS na wa serikali ya Somalia kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono juhudi zao.

Katika sehemu moja ya matamshi yake hayo, Pobee amesema: "Nimevutiwa na kustaajabishwa sana na hali niliyoiona Somalia. Nchi hii imepiga hatua kubwa. Nilikuweko nchini humo miaka kadhaa iliyopita na hivi sasa ninaona maendeleo tofauti na hali ilivyokuwa miaka iliyopita." Licha ya uharibifu mkubwa wa vita vya ndani, lakini Somalia inaleta matumaini ya kuwa na utulivu wa kudumu

Amesema: "Ninataka kumhakikishia kila mmoja wenu kwamba tumejifunza mambo mengi kutoka kwenu. Ninaahidi kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono juhudi zenu nchini Somalia.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Somalia, Ali Mohamed Omar amewashukuru washirika wa kimataifa kwa mchango wao katika maendeleo ya nchi hiyo.

"Somalia isingekuwa Somalia ya leo bila ya msaada wenu nyote," amesema na kuongeza kuwa: "Somalia imetoka mbali."

Naye Mohammed El-Amine Souef, mwakilishi maalumu wa Mkuu wa Kamisheni ya AU huko Somalia ambaye pia ni mkuu wa ATMIS amesema: "Tumekuwa na mkutano wenye tija na maafisa wa Ofisi ya Usaidizi wa Umoja wa Mataifa hapa Somalia. Tumekuwa na mazungumzo pia na makamanda wetu wa sekta mbalimbali na tumejadiliana ni jinsi gani tunaweza kushughulikia suala la mafuriko lililosababishwa na mvua za El Nino."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live