Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yataka ukomo Serikali mbili Libya

Ujumbe Wa UN Libya Umeelezea Wasiwasi Wa Watu Kuendelea Kutekwa UN yataka ukomo Serikali mbili Libya

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amesema kuwa, kukomeshwa hali ya kuweko serikali mbili nchini humo na kupatikana amani na utulivu wa kudunu ni jambo la dharura na lenye umuhimu mkubwa.

Kamati ya kuainisha sheria za uchaguzi inayoundwa na wajumbe sita wa Baraza Kuu la Majimbo la Libya na Bunge, kwa muda sasa linaendelea na vikao katika mji wa Benghazi wa magharibi mwa Libya kwa shabaha ya kufanyia marekebisho kipengee cha Azimio la Katiba kwa ajili ya kuweka msingi imara wa sheria za uchaguzi za nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Azimio hilo la Katiba linatambuliwa kuwa ndiyo marejeo makuu ya sheria ya uchaguzi ya Libya.

Abdoulaye Bathily, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amenukuliwa na televisheni ya Aljazeera akisema kuwa, sheria ya uchaguzi iliyopendekezwa na kamati ya 6+6 inaweza kuwa hatua nzuri ya kusonga mbele katika utatuzi wa migogoro ya Libya.

Ameongeza kuwa, tab'an baadhi ya vipengee vya pendekezo hilo vinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuepuka kuzusha mapigano na fujo za kisiasa kwa sababu ya uchaguzi.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa ametilia mkazo pia kushirikishwa pande zote katika zoezi hilo ili kuhakikisha kunapatikana sheria zinazozingatia pande zote na watu wa kada na matabaka yote.

Amezungumzia pia madhara ya mgogoro wa Sudan kwa Libya na kusema kuwa, mgogoro huo wa nchi jirani una madhara mengi kwa Libya kama ulivyo na madhara chungu nzima kwa nchi nyingine zinazopakana na nchi hiyo.

Tangu alipopinduliwa Muammar Gaddafi mwaka 2011 hadi hivi sasa, Libya haijawahi kuwa na utulivu wa kudumu na wa kuaminika kutokana na uingiliaji wa madola ya kiistikbari kama Marekani na madola ya kieneo.

Tangu mwaka 2014 Libya inatawaliwa na serikali mbili hasimu ambapo mapigano ya mwisho kabisa yaliyopiganwa na pande hizo mbili ni yale yaliyomalizika mwaka 2020.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live