Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa serikali ya Sudan kuchunguza tisho la mauaji ya afisa wake wa ngazi ya juu nchini humu humo.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea hofu kuhusiana na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mwanaume mmoja anauliza iwapo kumuua mwanadiplomasia wake Volter Perthes ni kinyume cha sheria.
Mwanaume huyo amekuwa akimtusi na kumkosoa muakilishi Mjumbe maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan katika maeneo ya kidini.
Alimshutumu Bw Perthes kwa kuwaondoa Waislamu wenye itikadi kali katika mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kurejesha mamlaka ya nchi kwa utawala wa kiraia.
Hatahivyo waandalizi wa tukio la kidini, wamejitenga na kauli za mwanaume huyo dhidi ya Bw Perthes.