Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yatahadharisha njaa kali Somalia

Watoto Njaa Somalia UN yatahadharisha njaa kali Somalia

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Adam Abdel Mawla ametoa wito wa msaada wa haraka wa kimataifa wakati baa la njaa likitishia maisha ya maelfu wa watu nchini Somalia.

Akizungumza na wanahabari katika Makao Makuu ya Umoja huo mjini New York, Abdel Mawla amesema Somalia iko hatarini kukumbwa na baa la njaa linaloweza kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Ameongeza kuwa, tangu mwanzo wa mwaka huu, hali ya ukame nchini Somalia imekuwa mbaya zaidi , na kwa sasa inakaribia kuwa janga kubwa.

Amesema, hivi karibuni baadhi ya sehemu nchini humo zilipata mvua kiasi, lakini hazikutosha kuondoa hali mbaya ya ukame, na kuonya kuwa, kuna hatari kuwa msimu ujao wa mvua pia utakuwa chini ya kiwango, na kuashiria mwaka wa tano wa uhaba wa mvua.

Alieleza kuwa Wasomali milioni 7.1, karibu asilimia 50 ya watu wote, wanakabiliwa na uhaba wa chakula. Ifikapo Septemba ijayo, alibainisha, watu 213,000 watakumbwa na janga la njaa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 160 tangu Aprili mwaka jana.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa alisema kuwa takriban watoto milioni 1.5 chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live