Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yatahadharisha kuhusu hatari ya maafa ya binadamu nchini Sudan

Ukrain Njaa UN yatahadharisha kuhusu hatari ya maafa ya binadamu nchini Sudan

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu amesema mzozo wa Sudan unaweza kulitumbukiza eneo zima kwenye maafa ya binadamu.

Martin Griffiths amesema kuwa vita na njaa vinaielekeza Sudan kwenye ukingo wa maangamizi kamili.

Griffiths ameongeza kuwa, mamia ya watoto nchini Sudan wako katika hatari ya kifo na utapiamlo.

Wakati huo huo, vyanzo vya habari jana Ijumaa viliripoti mapigano makali kati ya jeshi la nchi hiyo na Vikosi vya Msaada wa Haraka katika miji ya Khartoum na Omdurman.

Martin Griffiths ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuanza tena kwa migogoro nchini Sudan na kusema kwamba, njia za usambazaji wa chakula katika nchi hii iliyokumbwa na vita zimefungwa, sambamba na kumalizika kabisa akiba ya chakula.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amezitaka pande zinazozozana "kusimamisha mapigano na kuruhusu operesheni za misaada ya kibinadamu."

Maelfu ya watu wameuawa na zaidi ya milioni 4 wamelazimika kuyahama makazi yao, haswa katika mji wa Khartoum na jimbo la Darfur tangu kuanza kwa mapigano kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Jeshi la Sudan (SAF) mnamo Aprili 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live