Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yashitushwa kuanza kwa mapigano tena Sudan

Manyanyaso Ya Kingono Yatawala Sudan UN yashitushwa kuanza kwa mapigano tena Sudan

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba "ametiwa wasiwasi sana" na mapigano mapya nchini Sudan, na kuonya kwamba njia za misaada zimezibwa huku chakula kikiendelea kuisha katika nchi hiyo yenye vita.

Martin Griffiths amesema mapigano yamekuwa makali sana huko Darfur Kusini na Kordofan Kusini, akizitaka pande zinazozozana "kusimamisha uhasama na kuruhusu utoaji wa misaada."

Griffiths ameandika kwenye X, jukwaa lililojulikana hapo awali kama Twitter kwamba, "Watu wengi wameuawa na maelfu kukimbia makazi yao. Njia za misaada zimezuiwa na akiba ya chakula imepungua."

Maelfu ya watu wameuawa na wengine zaidi ya milioni 4 kufurushwa makwao tangu kuanza kwa vita kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Jeshi la Sudan (SAF) mnamo Aprili 15, haswa huko Khartoum na jimbo la Darfur.

Wafanyakazi 19 wa kutoa misaada wameuawa tangu mapigano yaanze zaidi ya miezi minne iliyopita, kulingana na Umoja wa Mataifa. Shirika hilo la kimataifa limeongeza kwamba makumi ya maghala na vifaa vingine vya kibinadamu vimeporwa.

Pande mbili zinazozozana zilitia saini makubaliano ya kibinadamu huko Jeddah, Saudi Arabia mnamo Juni ambayo yaliruhusu kufunguliwa korido za kibinadamu ili kupeleka msaada kwa raia. Hata hivyo, mapatano hayo yamekiukwa mara kwa mara na pande hizo mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live