Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yasema utapiamlo umeongezeka miongoni mwa wanawake wajawazito

UN Yasema Utapiamlo Umeongezeka Miongoni Mwa Wanawake Wajawazito UN yasema utapiamlo umeongezeka miongoni mwa wanawake wajawazito

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: Voa

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema kwamba utapiamlo umekithiri miongoni mwa wanawake wajawazito pamoja na wale wananaonyonyesha.

Hali hiyo inasemekana kuongezeka kwa asilimia 25 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, katika mataifa 12 yalioathiriwa na kupanda kwa bei za vyakula kutokana na vita vya Ukraine.

Utafiti kwenye mataifa 10 ya kiafrika na mawili ya Mashariki ya Kati, ambayo yameathiriwa zaidi umetumika kwenye ripoti hiyo ya UNICEF ya Jumanne, kabla ya maadhimisho ya Jumatano, ya siku ya kimataifa ya wanawake.

Ripoti imeongeza kusema kwamba ukosefu wa lishe bora miongoni mwa wajawazito na wale wanaonyonyesha huenda ukapelekea kushuka kwa kinga dhidi ya maradhi, pamoja na matatizo wakati wa kujifungua.

Baadhi ya mataifa yaliyopo chini ya jangwa la Sahara yameonyesha kuwa ni viwango vya juu vya vifo vya watoto wa kuzaliwa kwenye tafiti za awali, vikisababishwa na matatizo mbalimbali.

Takriban watoto milioni 51 waliopo chini ya umri wa miaka miwili kote ulimwenguni ni wafupi kuliko wanavyofaa kuwa kwa umri wao, kutokana na utapiamlo, na nusu yao huathiriwa wakiwa tumboni au katika miezi 6 ya kwanza ya maisha.

Wasichana walioathiriwa wameongezeka kutoka milioni 5.5 mnamo mwaka wa 2020 hadi milioni 6.9 mwaka jana, katika nchi kama Burkina Faso, Chad, Ethiopia, Kenya, Mali, Niger, Nigeria, Somalia, South Sudan, Sudan, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Chanzo: Voa