Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yaonya uwepo wa ISIS mapinduzi Afrika

Magaidi ISIS.jpeg UN yaonya uwepo wa ISIS mapinduzi Afrika

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa kundi la kigaidi la DAESH (ISIS) limeongeza maradufu idadi ya maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake nchini Mali.

Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti ya Al-Yaumu-Saabii, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wametangaza kuwa, katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja magaidi wa Daesh wameongeza takribani maradufu idadi ya maeneo wanayoyadhibiti nchini Mali.

Sambamba na hayo, makundi mengine yenye misimamo mikali yenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda, yameitumia fursa ya kudhoofika makundi yanayobeba silaha nchini Mali yaliyotia saini mkataba wa amani wa 2015 ili kujizatiti zaidi kijeshi na kuhodhi maeneo.

Imeelezwa katika ripoti hiyo ya wataalamu wa UN kwamba, Daesh na makundi yenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda yamepata nguvu zaidi; na magaidi wa Daesh wamehama kutoka kaskazini mwa Mali ambayo ni sehemu kavu na isiyo na maji wala nyasi na kuhamia katikati mwa nchi hiyo.

Rais wa zamani wa Marekan Donald Trump, aliwahi kukiri huko nyuma kwamba nchi hiyo ndiyo iliyopelekea kuibuka makundi ya kigaidi ikiwa ni pamoja na DAESH (ISIS) katika nchi za Syria na Iraq.

Ikumbukwe kuwa, mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 kwa uvamizi mkubwa wa makundi ya kigaidi yaliyokuwa yakiungwa mkono na Marekani na washirika wake, lengo likiwa ni kubadilisha mlingano wa nguvu za kijeshi katika eneo la Asia Magharibi kwa manufaa ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Miaka miwili baada ya kuanza machafuko na mapigano nchini Syria, mnamo Aprili 2013, kundi la kigaidi la ISIS lilitangaza uwepo wake nchini humo na kuanza kuvutia wanachama.

Mnamo mwaka 2017, na baada ya miaka mitatu ya mapigano, Iraq ilitangaza ushindi dhidi ya kundi la kigaidi la DAESH (ISIS), lakini baadhi ya wanachama na vikundi vidogovidogo vya kundi hilo la kigaidi vingaliko katika baadhi ya maeneo ya Iraq, Syria na baadhi ya nchi za Afrika vikiendelea kuendesha harakati zao.

Kwa mujibu wa ripoti rasmi, hadi sasa Marekani imeshatoa silaha na vifaa vyenye thamani ya mabilioni ya dola kwa magaidi wa ISIS walioko Syria na Iraq.../

Chanzo: www.tanzaniaweb.live