Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yaonya kuzorota uchumi Sudan Kusini

Sudan Kusini Uchumi Kuzorota UN yaonya kuzorota uchumi Sudan Kusini

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini (UNMISS) umetahadharisha kuhusu kuzorota uchumi wa nchi hiyo kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchi jirani ya Sudan ambayo ndio mshipa wa uhai wa Sudan Kusini.

Nicholas Haysom, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa UNMISS amesisitiza kuwa, shambulio dhidi ya bomba la mafuta ambalo ni la kusafirishia mafuta ya Sudan Kusini kuelekea soko la kimataifa kupitia Sudan, litazorotesha uchumi wa Sudan Kusini.

Haysom amesema hayo mbele ya waandishi wa katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba na kuongeza kwa kusema: "Tunafahamu kabisa kwamba moja ya hatari kubwa ambayo Sudan Kusini inakabiliana nayo ni shambulio kwenye bomba la mafuta yake huko Sudan, ambalo litakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Sudan Kusini."

Aidha amesema: "Sudan Kusini kwa kweli haiwezi kustahimili mshtuko mwingine mkubwa. Hadi sasa, mshituko huo haujatokea, lakini vita vinavyoendelea nchini Sudan ni kengele ya hatari kwa Sudan Kusini inayoiwajibisha kufanya lolote inalowezekena ili kuhakikisha amani inapatikana." Nicholas Haysom,

Haysom ametoa mwito wa kurejeshwa amani nchini Sudan haraka iwezekanavyo, akionya kwamba mgogoro huo unaweza kuzidisha maafa ya kibinadamu Sudan Kusini.

Vile vile ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono Sudan Kusini katika kukabiliana na mgogoro unaotokana na mzozo wa Sudan, akibainisha kuwa vita vya Sudan vimesababisha kupanda bei ya vyakula Sudan Kusini.

Amesema: "Mgogoro wa chakula umeongezeka Sudan Kusini, na uwezo wa kimaisha wa kaya zilizoko hatarini kupata chakula cha kukidhi mahitaji ya kimsingi umepungua. Harakati za biashara ya mipakani zimepungua sana na hivyo kupelekea kuweko uhaba wa bidhaa za chakula Sudan Kusini."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live