Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yaonya kuhusu kuongezeka kwa mizozo ya kikabila nchini DRC

Wansjeshi Butubd Fmdrcccc.jpeg UN yaonya kuhusu kuongezeka kwa mizozo ya kikabila nchini DRC

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, Volker Turk, mwishoni mwa wiki iliyopita, ameonya kuhusu kuongezeka kwa mizozo ya kikabila na vurugu nyingine nchini DRC, baada ya uchaguzi wa mwaka uliopita.

Turk amesema maeneo ambayo anahofia matukio hayo yanaweza kujitokeza ni kwenye jimbo la Kivu Kaskazini na Kusini, lakini pia mikoa ya Kasai na Katanga.

Kauli yake anaitoa baada ya tume ya uchaguzi, mwanzoni mwa wiki hii kumtangaza Felix Tshisekedi, kuwa mshindi wa uchaguzi wa Desemba 20, mwaka jana ambapo anatokea Kasai wakati mpinzani wake Moise Katumbi, akitokea eneo la Katanga.

Turk, ameziomba mamlaka nchini humo kuchunguza kwa makini na kwa uwazi, ripoti zote za arafa za chuki na uchochezi na kuhakikisha wahusika wanaojaribu kuchcohea machafuko ya kikabila wanawajibishwa.

Uchaguzi huu ambao umepingwa na upinzani, ulikumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo za kiufundi, na kufikia sasa tume ya uchaguzi CENI imetangaza matokeo ya urais, huku matokeo ya wabunge wa kitaifa na mikoa, kadhalika madiwani yakisubiriwa, ambapo pia ikifuta matokeo ya wagombea zaidi ya 80.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live