Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yaonya athari za mvua Somalia

Mafuriko Ya Somalia UN yaonya athari za mvua Somalia

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetahadharisha kuwa mvua kubwa na zisizo za kawaida zilizopewa jina la mvua za Gu pamoja na mafuriko yanayotarajiwa kutokea katika wilaya 22 za Somalia yanatabiriwa kuwa yatawaathiri takriban watu 770,000 nchini humo.

OCHA imesema kuwa, mvua za Gu zinazoanzia mwezi Aprili hadi Juni zimeanza kunyesha katika mikoa mingi ya Somalia ambayo tayari mvua kubwa zinanyesha katika baadhi ya maeneo, lakini hakuna mafuriko ya ghafla au mito iliyoripotiwa kufurika hadi hivi sasa.

Katika taarifa yake ya karibuni kabisa na ambayo imetolewa mjini Mogadishu, OCHA imesema, "Wanaharakati wa masuala ya kibinadamu wameandaa mpango wa kupunguza athari zinazotarajiwa kusababishwa na mvua za Gu, lakini wanahitaji msaada wa haraka kuhakikisha wanaokoa watu kwa wakati mwafaka.

Kwa mujibu wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa, boti takriban 51 zimepatikana kwa ajili ya kusaidia kuhamisha watu na kutoa msaada katika maeneo yaliyoko hatari zaidi yaani yake ya kando ya mito ya Shabelle na Juba. Limesema, kuna hatari mawasiliano yakakatika kutokana na mvua hizo na ikawa ni vigumu sana kuyafikisha misaada maeneo ambayo yatakuwa hayafikiki kutokana na njia kukatwa na mafuriko.

Katika upande mwingine lakini shirika la OCHA limesema kuwa, mvua hizo zimeleta ahueni kwa wafugaji na wakulima kilimo kote nchini Somalia kwani zitawasaidia kwa malisho ya wanyama wao na kuwa na akiba nzuri ya maji kwa ajili ya kilimo.

Mwishoni mwa mwaka jana 2023, mvua kubwa zilizopewa jina la Deyr ambazo hunyesha kuanzisha mwezi Oktoba hadi Desemba zilisababisha mafuriko na kupelekea watu milioni 1.6 kuyahama makazi yao. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live