Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yamwaga mabilioni haya Somalia

Displaced Somali People UN yamwaga mabilioni haya Somalia

Sun, 27 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu limetoa dola milioni 25 sawa na Tsh. bilioni 5.75 kwa ajili ya kutoa msaada wa haraka kwa jamii zilizokumbwa na ukame nchini Somalia.

Bw Adam Abdelmoula, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Misaada ya Kibinadamu nchini Somalia, Alhamisi alisema fedha kutoka Mfuko wa Kibinadamu wa Somalia (SHF) zitatumika kusambaza chakula cha msaada na maji katika maeneo ya mbali ya Jubbaland na Puntland.

Alisema kuwa mgao huo unakamilisha dola milioni 17 ambazo zilitolewa hivi majuzi kutoka Mfuko Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Dharura (CERF) ili kukidhi mahitaji ya haraka ya jamii zilizoathiriwa na ukame.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live