Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yakosoa vikali kitendo cha askari wa Israel cha kuuvunjia heshima Msikiti

Israel Haina Nia Ya Kukaa Muda Mrefu Gaza   Waziri Wa Ulinzi UN yakosoa vikali kitendo cha askari wa Israel cha kuuvunjia heshima Msikiti

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umesema kitendo cha kuuvunjia heshima msikiti kilicofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni jambo lisilovumilika. Kwa mujibu wa IRNA, kufuatia kusambazwa mkanda wa video unaowaonyesha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wakifanya ibada zao za Kiyahudi ndani ya msikiti katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesisitiza kuwa vitendo hivi vinakinzana na staha ya umma.

Dujarric ameongeza kuwa, maeneo ya kidini lazima yaheshimiwe na hayawezi kufanyiwa dharau na kuvunjiwa heshima kwa namna yoyote ile.

Matamshi hayo ya msemaji wa Umoja wa Mataifa yametolewa baada ya waziri wa usalama wa taifa wa utawala wa Kizayuni wa mrengo mkali wa kulia wenye misimamo ya chuki Itamar Ben-Gvir kuweka kwenye mtandao wa kijamii mkanda wa video unaowaonyesha wanajeshi wa utawala huo haramu wakifanya ibada za Kiyahudi ndani ya msikiti mmoja huko Jenin. Stephane Dujarric

Katika mkanda huo wa video anaonekana mwanajeshi wa Israel akisoma dua ya Kiyahudi kwa kutumia kipaza sauti cha msikiti. Imedaiwa kuwa askari hao walioonekana kwenye video hiyo wameadhibiwa.

Mnamo tarehe 7 Oktoba, makundi ya Muqawama ya Palestina yalianzisha operesheni ya kushtukiza Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza (kusini mwa Palestina) dhidi ya vituo vya kijeshi vya utawala wa Kizayuni; na katika hatua ya kulipiza kisasi, kufidia kushindwa kwake na kusimamisha operesheni za makundi ya Muqawama, utawala haramu wa Israel ulianzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya maeneo ya makazi ya watu, vituo vya matibabu na majengo ya kiutamaduni ya Ukanda wa Gaza ambayo hadi sasa yamepeleka kuuawa shahidi zaidi ya Wapalestina 18,000.

Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Misaada ya Kibinadamu (OCHA), karibu asilimia 90 ya wakazi wa Gaza wamebaki bila makazi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live