Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yaja na mpango mpya wa Uchaguzi Mkuu Libya

Kuraaa.png UN yaja na mpango mpya wa Uchaguzi Mkuu Libya

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametangaza kuanza mpango mpya utakaorahisisha kufanyika uchaguzi wa rais mwaka huu nchini humo.

Shirika la habari la Anadolu limeripoti habari hiyo na kumnukuu Abdoulaye Bathily, akitangaza habari hiyo Jumamosi wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tripoli na kuongeza kwamba anapanga kuzindua mpango mpya wa kuhakikisha kuwa pande husika za Libya zinakutana na kujadiliana njia za kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika mwaka huu.

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Libya amesema: Tume kuu maalumu itaundwa. Wajumbe wa tume hiyo hawataamuliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL), bali watateuliwa na taasisi za serikali, mashirika ya kijamii na pande husika. Vyama vya Libya vitawasilisha wagombea wao na ujumbe wa usaidizi utafanya mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa kati na kati.

Abdoulaye Bathily aidha amesema kuwa, tume hiyo itafanya kazi kwa bidii na kwa nia moja na ndiyo itakayoamua muda wa kufanyika uchaguzi huo mwaka huu.

Mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya vile vile amesema, Tume hiyo haitofanya ubaguzi wowote na itatoa suluhisha linaloendana na mazingira ya Libya.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kwa mara nyingine amesisitizia wajibu wa kuweko msimamo mmoja hususan baina ya asasi za kiutawala likiwemo jeshi kuhusu utekelezwaji wa mpango wa kuondoka vikosi vya kigeni na wanamgambo katika nchi hiyo kama hatua moja mbele ya kupatikana amani na utulivu wa kudumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live