Thu, 16 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya nyuklia linasema kuwa linajaribu kutafuta karibu Tani 2.5 za madini ya 'Uranium' ambayo yametoweka katika eneo ambalo haliko chini ya udhibiti wa serikali ya Libya.
Imeelezwa kuwa wakaguzi waligundua kuwa madumu 10 yaliyokuwa na madini hayo ambayo hutumika kutengeneza Silaha za Nyuklia hayaonekani katika ghala yalimokuwa yamehifadhiwa.
Wakaguzi hao wanahofia kuwa Uranium hiyo inaweza kusababisha hatari ya kimionzi na wasiwasi wa usalama wa nyuklia
Chanzo: www.tanzaniaweb.live