Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yahimiza misaada zaidi kwa ajili ya Sudan

Baraza La Usalama La Umoja Wa Mataifa Lataka Wanajeshi Kuuachilia Mji Wa El Fasher Sudan UN yahimiza misaada zaidi kwa ajili ya Sudan

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed, ametoa wito wa kutolewa misaada zaidi kwa Sudan akisisitiza kwamba, juhudi zilizofanywa hadi sasa katika uga huo hazijatosha kupunguza mateso wanayopata raia wa nchi hiyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameyasema hayo wakati wa ziara yake kwenye kituo cha mpakani cha Adre kilichoko nchini Chad kushuhudia upitishaji wa misafara ya misaada ya kibinadamu.

Katika ziara yake hiyo, Amina Mohammed ametoa wito pia wa kutekelezwa azimio la kusitisha mapigano nchini Sudan.

Wakati wa mazungumzo ya hivi majuzi mjini Geneva, pande zinazozozana zilipiga hatua ndogo katika suala la kumaliza mapigano lakini ziliahidi kuruhusu misaada ya kibinadamu kupita katika maeneo mawili muhimu ya mpaka.

Bi Amina Mohammed (wa pili kulia) akiwa kwenye kivuko cha Chad Vyombo vya habari vimeripoti kuwa vimeshuhudia misafara ya misaada ya kibinadamu ikivuka mpaka na kuingia jimbo la Darfur nchini Sudan wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Siku ya Alkhamisi, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP lilieleza katika taarifa kwamba malori yake yamesafirisha zaidi ya tani 630 - zinazotosha watu karibu 55,000 - kutoka Chad hadi eneo la Darfur.

Hata hivyo akiwa katika ziara yake huko Adre Bi Amina Mohammed alisema kiwango hicho ni kidogo kulinganisha na kinachohitajika ili kukabiliana na mateso wanayopata raia wa Sudan.

Alisema Umoja wa Mataifa ulikuwa na uwezo wa kufadhili takribani asilimia 25 hadi 30 ya mahitaji, na akaongezea kwa kusema: "ahadi zilizotolewa na serikali zinahitaji kutimizwa ili tuweze kuwasaidia watu wahitaji duniani."

Mapigano yalizuka nchini Sudan mwezi Aprili 2023, yakihusisha jeshi la taifa linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka vya naibu wake wa zamani, Mohamed Hamdan Dagalo.

Mashirika ya misaada yanasema mapigano hayo yamezuia misaada ya kibinadamu kuwafikia Wasudan milioni 25 wanaokabiliwa na njaa kali.../

Chanzo: www.tanzaniaweb.live