Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN yaani shambulio dhidi ya walinda amani DRC

Guterres Aendelea Kusisitiza Kusimamishwa Mapigano Gaza UN yaani shambulio dhidi ya walinda amani DRC

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulizi lililopelekea kujeruhiwa wanajeshi wanane wa umoja huo wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakati wa mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Serikali.

Tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi katika eneo la Sake, kilomita 20 tu kutoka Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Walinda amani waliojeruhiwa, ambao walikuwa sehemu ya Operesheni Springbok iliyoanzishwa Novemba mwaka jana kulinda raia katika eneo hilo, wamepata majeraha huku mapigano yakiendelea, ambapo wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakisaidia vikosi vya Serikali ili kuwalinda raia walio hatarini.

Katika taarifa yenye maneno makali iliyotolewa na Msemaji wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani shambulizi hilo akisisitiza kuwa linaweza kuwa uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa.

Zaidi ya hayo, Guterres amesisitiza ulazima wa M23 kujiondoa kabisa katika eneo ililokalia na kuendana na makubaliano yaliyoainishwa katika taarifa ya Luanda ya Novemba 2022, ili kulinda uhuru na umoja wa eneo lote la ardhi ya DRC. Askari wa MONUSCO

Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO naye pia amelaani mashambulio hayo.

Bi. Keita amesema mmoja wa walinda amani waliojeruhiwa amepata majeraha makubwa na wote wamehamishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu yanayofaa.

Walinda amani hao walikuwa wametumwa kwa wiki kadhaa kama sehemu ya Operesheni Springbok katika eneo lenye machafuko la Kivu Kaskazini, wakifanya kazi kwa pamoja na wanajeshi wa Serikali katika operesheni za kijeshi. Bi. Keita amethibitisha kujitolea kwa MONUSCO kusaidia uchunguzi kwa matumaini ya kuwafikisha waliohusika mbele ya sheria.

Katibu Mkuu wa UN na Mwakilishi wake Maalumu wamesisitiza azimio la MONUSCO la kutekeleza zaidi jukumu lake la ulinzi wa raia ililokabidhiwa na Baraza la Usalama na kufanya kazi pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama vya DRC kuimarisha doria za pamoja na za upande mmoja ili kulinda raia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live