Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN wahuzunishwa na hatua mbaya za makundi ya Libya

Libya 13 Mapigano UN wahuzunishwa na hatua mbaya za makundi ya Libya

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umeelezea kuhuzunishwa kwake na hatua za upande mmoja za hivi karibuni za pande hasimu na baadhi ya vyama vya siasa nchini humo.

Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kusema kuwa unafuatilia kwa hofu na wasiwasi vitendo vya upande mmoja vya hivi karibuni vya makundi na taasisi za kisiasa za Libya katika maeneo ya mashariki, magharibi na kusini mwa nchi hiyo.

Sehemu moja ya taarifa ya UNSMIL imesema: "Katika mazingira ya hivi sasa, vitendo hivi vya upande mmoja vinaongeza tu mvutano, kudhoofisha kuaminiana na kuzidisha migawanyiko ya kitaasisi na mifarakano miongoni mwa wananchi wa Libya."

Taarifa hiyo imesisitizia udharura wa kuweko maafikiano, mazungumzo na mshikamano baina ya wananchi wa Libya na umewakumbusha viongozi na taasisi zote za kisiasa ahadi na wajibu wao chini ya Mkataba wa Kisiasa wa Libya na maazimio yote muhimu ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hasa azimio nambari 2702 lwa mwaka (2023).

Baraza la Wawakilishi au Bunge lenye makao yake Mashariki mwa Libya siku ya Jumatatu lilikataa uamuzi wa Baraza la Uongozi lenye makao yake makuu mjini Tripoli wa kuunda chombo kipya cha kusimamia kura za maoni na masuala ya kitaifa na kutaka chombo hicho kifutiliwe mbali.

Libya imeendelea kuwa na migawanyiko hatari ya kisiasa kwa zaidi ya muongo mmoja sasa baada ya kupinduliwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, mwaka 2011.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live