Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN kusaidia waathirika wa mafuriko DRC

Mafuriko Un Msaada DRC.png UN kusaidia waathirika wa mafuriko DRC

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mikoa tisa kati ya 12 ya Congo imeathiriwa na mfululizo wa mafuriko tangu mwezi Oktoba mwaka jana, na kuathiri angalau watu milioni 1.7. Baadhi ya waathiriwa 350,000 wanahitaji usaidizi wa dharura. Kutokana na hali hiyo, serikali na Umoja wa Mataifa walitengeneza mpango wa kukabiliana na hali hiyo unaokadiriwa kufikia dola milioni 26.

Umoja wa Mataifa tayari umekusanya dola milioni 3.6. Chris Mburu, mratibu wa mfumo wa Umoja wa Mataifa, anaeleza jinsi ufadhili huo utatumiwa: “Jibu wa msaada huu utazingatia mikoa minne: Likouala, Cuvette, Plateaux na Pool, ili kutoa msaada katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi . Shughuli zitajumuisha afya, lishe, elimu, usalama wa chakula na majibu ya dharura ya ulinzi. "

Kulingana na Umoja wa Mataifa, angalau wanafunzi 27,000 katika maeneo yenye mafuriko hawako tena shuleni; Heka 2,300 za ardhi ya kilimo na miti ya matunda viko kwenye maji. Mamia ya wanawake hujifungua kwenye boti au katika vyumba vya upasuaji vilivyokumbwa na mafuriko. Kuanzia sasa, watu wanahofia kuzuka kwa magonjwa yanayotokana ya kuambukiza kama vile Kipindupindu, magonjwa mengine ya ngozi.

Chris Mburuanasema kila mtu lazima ajitokeze kusaidia waathiriwa: "Tunaomba msaada kutoka kwa kila mtu, ikiwa ni pamoja na sekta ya kibinafsi na mshikamano, ili misaada ifike haraka katika maeneo yote yaliyoathirika", aamebaini.

Mafuriko yanatokea mara kwa mara nchini Kongo, lakini kiwango cha sasa cha uharibifu ni janga, yanasema mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu ambayo yanatarajia hali mbaya zaidi katika siku zijazo, kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live