Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN kupiga kura kuhusu kutumwa kwa polisi wa Kenya nchini Haiti

UN Kupiga Kura Kuhusu Kutumwa Kwa Polisi Wa Kenya Nchini Haiti UN kupiga kura kuhusu kutumwa kwa polisi wa Kenya nchini Haiti

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu linatarajiwa kupigia kura azimio litakaloshuhudia kikosi cha kimataifa kikiongozwa na Kenya kutumwa Haiti ili kukomesha ongezeko la ghasia za magenge.

Baraza hilo lenye wanachama 15 linatazamiwa kuunda mfumo na kuidhinisha kutumwa kwa kikosi hicho kwa mwaka mmoja, na kupitiwa tena baada ya miezi tisa.

Iwapo itaidhinishwa na Umoja wa Mataifa, Kenya itapeleka maafisa 1,000 wa polisi nchini Haiti ifikapo Januari mwaka ujao. Bahamas, Jamaica na Antigua and Barbuda wamesema watashiriki katika misheni hiyo.

Kikosi hicho kitasaidia kutoa mafunzo kwa polisi wa Haiti na kujenga upya miundombinu muhimu ambayo imekuwa ikizidiwa na magenge ya wahalifu.

Marekani imeahidi kutoa $100m (£82m) kusaidia misheni hiyo.

Haiti imekumbwa na ghasia za magenge kwa miongo kadhaa lakini wimbi la ukatili liliongezeka baada ya mauaji ya Julai 2021 ya Rais Jovenel Moïse.

Magenge yamechukua udhibiti wa maeneo makubwa ya nchi, yakiendesha ugaidi kwa wakazi na kuua mamia.

Chanzo: Bbc