Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN kuisaidia Tunisia kulinda usalama

Tunisia Amani Un UN kuisaidia Tunisia kulinda usalama

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limetiliana saini na Tunisia ili kuisaidia nchi hiyo kuenesha mageuzi makubwa ya kiusalama.

Hayo yametangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia ambayo imeongeza kuwa, amuzi huo umechukuliwa wakati wa mkutano uliofanyika nchini humo kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tunisia Kamel Feki na mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Tunisia, Celine Moyroud.

Feki ametilia mkazo dhamira ya nchi yake ya kuimarisha ushirikiano katika mageuzi ya usalama kwa kuzingatia viwango na masharti ya makubaliano na mikataba ya kimataifa.

Maafisa hao wawili pia wamesisitizia haja ya kutiwa nguvu polisi jamii katika majimbo mengi zaidi ya Tunisia ili kujenga uaminifu kati ya raia na vyombo vya usalama. Wimbila wahamiaji haramu ni kubwa nchini Tunisia

Hayo yamekuja baada ya mamlaka za usalama nchini Tunisia zimeanzisha kampeni maalumu ya usalama katika jimbo la kusini mashariki la Sfax ili kukomesha wimbi la wahamiaji haramu.

Mwezi Septemba uliopita, vyombo vya Habari vya Tunisia viliripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wahamiaji haramu wanatumia siku kama hizi kujipenyeza kwa wingi katika jimbo hilo kwa ajili ya kuelekea kwenye fukwe za barani Ulaya kwa tamaa ya kupata maisha bora.

Serikali ya Tunisia ilitangaza kuwa, kampeni hiyo ya usalama imetokana na maagizo ya Rais Kais Saied wa Tunisia na inalenga kukomesha wimbi kubwa la wahamiaji haramu ambalo kwa mujibu wa shirika rasmi ila habari la Tunisia, (TAP), wimbi hilo kubwa halikubaliki kabisa. Sambamba na kuanza kampenzi hiyo, askari wa Tunisia walikamta wakuu 16 wa mitandao ya magendo ya wahamiaji haramu ingawa wimbi hilo halijapungua hadi hivi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live