Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Zaidi ya watu milioni 7.4 wamekimbia vita nchini Sudan

Unmaisha Magumu UN: Zaidi ya watu milioni 7.4 wamekimbia vita nchini Sudan

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa, idadi ya watu waliokimbia vita nchini Sudan imeshapindukia milioni 7.4.

Katika taarifa yake ya jana, OCHA imesema: "Zaidi ya watu milioni 7.4 wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan tangu mapigano yalipozuka kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na wapiganaji wa Msaada wa Haraka (RSF) mnamo Aprili 15, 2023."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, idadi ya watu waliokimbia makazi yao nchini Sudan imeongezeka kwa takriban 611,000 katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, na wengi wao wamekimbia makazi yao kutoka Gezira na majimbo mengine ya Sudan.

Pia imesema: "Kutanuka mapigano kati ya SAF na RSF katika maeneo ya katikati na mashariki mwa Sudan ambayo ni maeneo ya uzalishaji wa mazao nchini humo - kumesababisha ongezeko kubwa la mahitaji ya kibinadamu."

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ukosefu wa usalama, uporaji, urasimu, mtandao duni wa mawasiliano yakiwemo ya simu, ukosefu wa fedha na wafanyakazi wachache wa masuala ya kiufundi na kibinadamu ni miongoni mwa masuala yanayoathiri vibaya zoezi la utoaji misaada nchini Sudan.

Sudan imekuwa ikishuhudia mapigano makali kati ya majenerali wa kijeshi wenye uchu wa madaraka ambao wanaongoza makundi mawili ya SAF na RSF tangu Aprili 15, 2023. Hadi hivi sasa mapigano hayo yameshasababisha zaidi ya watu 12,000 kuuawa kama zinavyoonesha takwimu wa OCHA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live