Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Zaidi ya watu 13,000 wameuawa katika vita vya Sudan

Wasudan Sudan UN: Zaidi ya watu 13,000 wameuawa katika vita vya Sudan

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 13,000 wameuawa na wengine 26,000 kujeruhiwa katika vita vinavyoendelea nchini Sudan tangu mwaka jana, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu imetangaza Jumapili.

Sudan ilikumbwa na vita kati ya Jeshi la Kitaifa, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni mkuu wa Baraza tawala la nchi hiyo, na kundi la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) tangu Aprili 2023.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilisema katika taarifa yake kwamba, "Takriban watu milioni 7.6 wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan tangu mapigano yazuke."

Kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya visa 9,700 vinavyoshukiwa kuwa kipindupindu, vikiwemo vifo 269 vinavyohusishwa, viliripotiwa nchini Sudan kufikia Januari 16.

Kamanda wa Vikosi vya Radiamali ya Haraka vya Sudan (RSF) Jenerali Mohammad Hamdan Dagalo (Hemedti) anasisitiza kuwa njia bora ya kuhitimisha mapigano nchini humo ni kuviunganisha vikosi hivyo na Jeshi la Sudan. Mapigano yalivyosababisha mgogoro wa wakimbizi Sudan

Hitilafu kati ya al-Burhan na Dagalo zilijitokeza baada ya kusainiwa mkataba wa kuunda kipindi cha mpito na kukabidhiwa madaraka kwa raia.

Jitihada za kieneo na kimataifa za kuwapatanisha mahasimu hao wawili wa Sudan vimefeli hadi sasa na vita hivyo vinatarajiwa kushadidi katika siku zijazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live