Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi Somalia

Kusini Magharibi Mwa Somalia UN: Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi Somalia

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku ya Jumatano yamesababisha watu 107,000 kuyahama makazi yao katika wilaya ya Baidoa ya kusini magharibi mwa Somalia.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, nyumba kadhaa zimefunikwa na maji yakiwemo makazi ya muda ya yaliyokuwa yamewapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 86,700 wa ndani huko Baidoa.

Sehemu moja ya taarifa ya OCHA imesema: "Mvua hizo zimenyesha ikiwa ni mwanzoni mwa msimu wa mvua za vuli unaoanza mwezi Oktoba hadi Desemba nchini Somalia. Hiyo ni ishara kwamba mvua za mwaka huu zitakuwa kubwa zaidi na kuna hatari ya kutokea janga la El-Nino nchini humo."

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mvua hizo kubwa na mafuriko yamekuja kufuatia misimu mitano ya ukame ambayo imesababisha vifo vya zaidi ya Wasomali milioni 1.4 na mifugo milioni 3.8 tangu katikati ya mwaka 2021. Mafuriko kusini mwa Somalia yamesababisha madhara makubwa

Serikali za mitaa huko Baidoa zinatayarisha zimetoa mwito kwa mashirika ya misaada ya kkibinadamu kusaidia kufikishiwa mahitaji ya dharura wahanga wa mafuriko hayo na kutoa msaada wa ziada kwa shughuli zinazoendelea hivi sasa za kuhudumia wakimbizi hao.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu milioni 1.2 na hekta milioni 1.5 za ardhi yenye tija wako katika hatari kubwa kutokana na mafuriko nchini Somalia. Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) lilisema siku ya Ijumaa kwamba linahitaji dola milioni 11.8 za Marekani ili kutia nguvu hatua za kukabiliana na hali hiyo, ikiwa ni pamoja na kuchora ramani ya maeneo yenye mafuriko kabla ya janga la El Nino kutokea nchini Somalia ingawa janga hilo ni nadra sana kushuhudiwa nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live