Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Zaidi ya Wasudan 800 waliuwawa mwanzoni mwa mwezi huu Darfur

Marekani Inaitaka RSF Ya Sudan Kuacha Kushambulia Maeneo Ya Raia Zaidi ya Wasudan 800 waliuwawa mwanzoni mwa mwezi huu Darfur

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa na madaktari wa Sudan wamesema wanamgambo wa RSF na makundi ya wanamgambo wa Kiarabu wamewauwa zaidi ya watu 800 katika mashambulizi waliyoyafanya katika mji mmoja ulioko katika jimbo la Darfur.

Mashambulizi hayo dhidi ya mji wa Ardamata, ulioko katika mkoa wa Magharibi mwa Darfur yalifanyika mwanzoni mwa mwezi huu na ndiyo mashambulizi ya hivi karibuni kabisa katika msururu wa matukio ya mauaji katika jimbo hilo, kufuatia mapigano kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa Kikosi cha Usaidizi wa haraka (RSF).

Mapigano ya kuwania madaraka nchini Sudan yalianza Aprili 15 kati ya vikosi vya Jeshi na vya Usaidizi wa Haraka RSF; na juhudi za upatanishi wa kimataifa za kumaliza vita na mapigano hayo na kuzileta pande zinazozozana kwenye meza ya mazungumzo hadi sasa hazijazaa matunda. Majenerali wawili wa Sudan wanaoendesha vita

Wakati huo huo, idadi ya watu wanaokimbia machafuko katika jimbo la Darfur huko Sudan inaripotiwa kuongezeka kufuatia wimbi jipya la mauaji ya kikabila.

Watu wanaokimbilia Chad kutoka Sudan, wanaelezea juu ya ongezeko jipya la mauaji ya kikabila katika jimbo la Darfur Magharibi, wanamgambo wa RSF walipoiteka kambi kuu ya jeshi katika mji mkuu wa jimbo hilo, El Geneina. Wanamgambo wa RSF wamekuwa wakipambana na jeshi rasmi tangu Aprili mwaka huu katika mzozo ambao umewalazimisha wakaazi wengi wa Darfur kuyahama makazi yao.

Umoja wa Mataifa umegusia juu ya uwezekano wa kushuhudiwa jinai dhidi ya binadamu huko Darfur na kutahadharisha kuwa mzozo unaoendelea jimboni humo umechukua mwelekeo wa kikabila katika eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live