Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN Yalaani mpango wa Uingereza wa kupeleka wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda

Waomba Hifadhi Iii UN watoa msimamo sakata la waomba hifadhi Rwanda

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Filippo Grandi, ametupilia mbali uamuzi wa serikali wa Uingereza wa kuwahamishia Rwanda watafuta hifadhi wanaokwenda nchini humo huku akisema makubaliano hayo ya kando kati ya nchi mbili hizo ni makosa.

Tamko la Grandi linakuja wakati majaji waandamizi wa Uingereza wakitangaza kuwa ndege ya kwanza ya serikali ya Uingereza ya kuhamishia wahajiri wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda inaweza kuondoka.

Jaji wa Mahakama Kuu nchini Rwanda alikataa pingamizi ya muda iliyotolewa Ijumaa ya kusitisha safari ya kwanza iliyokuwa ianze leo Jumanne, na kwa mujibu wa ripoti, Mahakama ya Rufani imekazia hukumu hiyo.

Mahakama itasikiliza kwa kina sera hiyo tata mwezi ujao.

“Kuhusu Rwanda, nafikiri tumekuwa wawazi katika wiki chache zilizopita na tunaamini kuwa hili ni kosa kwa sababu lukuki,” amesema Kamishna Mkuu huyo wa UNHCR.

Akisisitiza kuwa Uingereza imetia saini Mkataba wa Kimataifa kuhusu Wakimbizi, Grandi amesema, “kujaribu ‘kuuza’ nje ya nchi wajibu uliomo kwenye mkataba huo ni kinyume na azma yoyote ya kimataifa ya kusaidiana majukumu.”

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi ameendelea kubainisha kuwa, Rwanda ilikuwa na historia ya kipekee ya kukaribisha na kusaidia maelfu ya wakimbizi kutoka DRC na Burundi, na akaongezea kwa kusema, nchi hiyo haina uwezo na miundombinu ya kuhudumia wakimbizi kwa kuzingatia mahitaji ya sasa.

Grandi amefafanua kwa kusema, “Ingekuwa ni kutoka Rwanda kwenda Uingereza, pengine tungaliweza kujadili, lakini hapa tunazungumzia, Uingereza, nchi ambayo ina mifumo na inahamishia jukumu lake kwa nchi nyingine, Rwanda.”

Halikadhalika, Mkuu wa UNHCR ametaka yafanyike mawasiliano zaidi na Ufaransa ambako ndiko wanakotoka wakimbizi wengi zaidi watakaoathiriwa na mpango huu wa kuwahamishia watafuta hifadhi Rwanda, akisema “Ufaransa ina mifumo ya kusaidia watafuta hifadhi.”

Sera hiyo ilipotangazwa, Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alisema mpango huo wa dola milioni 160 utaokoa maisha ya wengi wa wahamiaji ambao mara nyingi hujikuta kwenye mikono ya wasafirishaji haramu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live