Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Watu milioni saba walikimbia makazi yao nchini DRC

GOMA DRC.png Watu milioni saba walikimbia makazi yao nchini DRC: UN

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa mapaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2023, watu milioni saba walikimbia makazi yao nchini DRC, wakiwemo milioni 2 na laki 5 katika jimbo la Kivu Kaskazini pekee.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za Binadamu, Human Rights Watch, limechapisha ramani yake inayoashiria maendeleo ya hali ya Haki za binadamu likitoa wito kwa Rais wa DRC, Félix Tshisekedi kuzingatia zaidi masuala ya haki za binadamu katika kipindi hiki cha muhula wake wa pili.

Katika Nyaraka zilizochapishwa hivi karibuni, Human Rights Watch imeitaka serikali ya Congo kuzingatia uhuru wa watu kujieleza na usalama wa raia katika maeneo yenye migogoro.

Thomas Fessy ni mtafiti mkuu wa shirika hilo nchini DRC.

“Kwa bahati mbaya sana ahadi nyingi zinaonekana kutotekelezwa ukizingatia kukamatwa kwa watu kiholela na vitisho kadhaa dhidi ya wanaharakati.” alisema Thomas Fessy ni mtafiti mkuu wa HRW nchini DRC.

Haya yanajiri wakati huu shambulio jipya linalohusishwa na kundi la Allied Democratic Forces (ADF), limesababisha vifo vya watu takriban 11 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika kijiji cha Kinyamusehe, umbali wa kilometa 25 kaskazini mwa jiji la Beni.

Kwa mujibu wa duru za usalama, waasi hao wenye uhusoano na Islamic State, walishambulio kijiji hicho usiku wa kuamkia Jumanne, wakati watu wamelala.

Kanali Ehuta Omeonga ni kiongozi wa wilaya ya Beni.

“Jeshi letu litaendelea kupambana hadi mwisho kuhakikisha raia wanapata amani.” alieleza Kanali Ehuta Omeonga, kiongozi wa wilaya ya Beni.

Kundi hili, ambalo ni moja ya makundi hatari zaidi yaliyoua watu wengi nchini DRC, lilitangaza kuwa mshirika lwa Islamic State mwaka 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live