Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Watu milioni 17.7 Sudan wanakabiliwa na njaa

Njaa Wakimbizi Wafa UN: Watu milioni 17.7 Sudan wanakabiliwa na njaa

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jana Ijumaa lilisema kuwa, watu milioni 17.7 kote nchini Sudan wanakabiliwa na "viwango vya juu vya uhaba wa chakula."

Idadi ya watu walioko hatarini zaidi wamerundikana katika majimbo yenye vita na ghasia, ikiwa ni pamoja na Darfur, Greater Kordofan na Khartoum, hasa katika maeneo makuu matatu ya mji mkuu huo, yaani Khartoum, Bahri na Omdurman.

Hayo yametangazwa na Adam Yao, naibu mwakilishi wa FAO nchini Sudan, na kuonya kwamba hali ya usalama wa chakula nchini Sudan ni mbaya na imepanda hadi "kiwango cha kutisha sana, kinachohitaji hatua za haraka na za pamoja."

Ametoa makadirio mapya akisema kuwa, watu hao milioni 17.7 wanakabiliwa na matatizo mengi ukiwemo mgogoro mbaya zaidi wa chakula ambao ulianza kuonesha makucha yakwe mwezi Oktoba mwaka huu wa 2023 na utaendelea hadi mwezi Februari 2024.

Wakimbizi wanapitisha kipindi kigumu sana

Katika jimbo la Khartoum, watu milioni 3.9 wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, ambapo kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa Darfur, takriban watu milioni 5.3 wako hatarini kukumbwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula jimboni humo.

Vita vya uchu wa madaraka kati ya majenerali wa kijeshi wanaoongozwa Jeshi la Sudan SAF na Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF vinaendelea kuinakamisha Sudan katika kona zote huku wahanga wakuu wa vita hivyo wakiwa ni raia wa kawaida.

Adam Yao, naibu mwakilishi wa FAO nchini Sudan pia amesema: "Watu wa Sudan wanahitaji kuungwa mkono hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote na hatua yetu ya haraka ya kulinda maisha ya jamii za vijijini za Sudan ni muhimu kabisa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live