Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Watu milioni 13 wanakabiliwa na njaa pembe ya Afrika

Njaa Afrika Watu milioni 13 wanakabiliwa na njaa pembe ya Afrika

Wed, 9 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema kwenye ripoti yake kwamba hali ya ukame katika eneo la Pembe ya Afrika imesababisha njaa kubwa kwa takriban watu milioni 13.

WFP imekadiria idadi hiyo ya watu wapatao milioni 13 wanaokabiliwa na janga la njaa kutokana na ukame katika nchi za Kenya, Somalia na Ethiopia.

WFP imesema eneo la Pembe ya Afrika limekumbwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miongo kadhaa.

Mkurugenzi wa WFP Kanda ya Afrika Mashariki Michael Dunford kutoka Nairobi amesema hali ya ukame inaziathiri jamii za wafugaji na wakulima kote katika nchi hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live