Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UN: Wanajeshi wa Burundi zaidi ya 1,000 watumwa kwa siri DRC

Wanajeshi Wa Burundi UN: Wanajeshi wa Burundi zaidi ya 1,000 watumwa kwa siri DRC

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo haijachapishwa iliyonaswa na shirika la habari la Reuters inaeleza kuwa wanajeshi wa Burundi zaidi ya 1,000 wametumwa kwa siri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu mwezi Oktoba mwaka huu.

Wanajeshi hao wa Burundi wameonekana wakiwa wamevalia sare za wanajeshi wa Kongo wakishirikiana katika mapambano dhidi ya kundi la waasi la M23. Waasi wa M23

Ikizinukuu duru za usalama na intelijinsia na zilizo karibu na jeshi la Kongo, ripoti hiyo ya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa wanajeshi hao walisafirishwa kwa ndege za jeshi la Kongo kutoka Burundi hadi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu Septemba 21 mwaka huu.

Serikali za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na jeshi la Kongo hadi sasa hazijatoa maelezo yoyote kuhusu ripoti hii tajwa. Ripoti hii kuhusu kutumwa kwa siri wanajeshi wa Burundi huko mashariki mwa Kongo ilisambazwa miongoni mwa wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 15 mwezi huu na kisha ilinaswa jana na shirika la habari la Reuters. Ripoti hii inatazamiwa kuchapishwa mwezi ujao wa Januari.

Ripoti hii inatupia jicho mkakati wa usalama wa Kongo mashariki mwa nchi hiyo, zaidi ya kutumwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa Kongo, ambao walikuwa wakiungwa mkono na kikosi cha kanda cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hadi mapema mwezi huu wa Disemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live